TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 29/07/2013

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limefanikia kukamata lita 600 za pombe haramu ya gongo, mitambo 11 na mapipa 134 ya (molasisi) ambayo ni malighafi inayotumika kutengeneza pombe hiyo.

Mafanikio hayo yametokana na operesheni maalumu ya msako iliyofanyika 27/07/2013 katika wilaya ya Kongwa, kijiji cha Kimero-Kiteto kata ya Lenjulu Tarafa ya Mlali wilaya ya Kongwa.

Pia Jeshi limefanikiwa kukamta debe 10 za Bhangi kwenye kijiji cha Garigari kitongoji cha Mfiro wilaya ya Mpwapwa ambapo debe 8 zimeteketezwa.

Alitekamatwa na pombe ya gongo, mitambo 11 na mapipa 134 ya molasisi ni TAITA S/O MASHAKA RASHIDI@Rashid, Mchaga, miaka 40, mkulima na makzi wa Kimero Kiteto Kongwa.

Waliokamatwa na Bhangi huko Mpwapwa ni;
1. FREDRICK S/O NGIMBA, mhehe, miaka 25, mkulima,
2. EMANUEL S/O NGIMBA, Mhehe, miaka 28, mkulima,
JUMA S/O NGIMBA, mhehe, miaka 46, mkulima wote wakazi wa kijiji cha Garigari.

Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kulipa tarifa zinazoleta mafanikio kama haya ya kupunguza uhalifu na madhara kwa afya za watu.

Imetolewa na;
DAVID A. MISIME-ACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA.