TAARIFA YA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jeshi la polisi mkoa wa Dododma linamtafuta NYERERE S/O BAKARI, Mrangi, Mkazi wa Wilayani Kondoa kwa tuhuma za kumuua Abdallah S/O YUSUPH MGUNDA, Miaka 25,Mrangi, Mfugaji wa kijiji cha Kwadelo Wilaya ya Kondoa,kwa kumpiga risasi zilizompata sehemu ya kifuani na kwenye mapaja kwa kutumia silaha inayodhaniwa ni gobore mnamo tarehe 23/07/2013 majira ya 02:00 HRS (saa nane uusiku).
      Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa ni ugomvi uliozushwa na mtuhumiwa kuwa marehemu alikuwa amelisha mifugo kwenye shamba lake.
     Aidha Mnamo tarehe 23/07/2013 majira ya 06:30 HRS (saa kumi na mbili na dakika thelathini asubuhi) huko Nkuhungu Manispaa ya Dodoma IMANI S/O FRANCIS, Miaka 28,Mgogo, Mkazi wa Nkuhungu alikutwa ameuawa katika eneo la Itega karibu na TANK LA MAJI kwa kupigwa na watu waliojichukulia sheria mikononi.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alishakuwa na tuhuma ya KUBAKA,Kujaribu kunyang'anya pikipiki na kujaribu kumpora mama mmoja pochi,ingawa matukio haya hayajawahi kuripotiwa polisi.