WANAHABARI MKOANI DODOMA WAPATA UONGOZI MPYA

Uongozi mpya wa chama cha waandishi wa habari Mkoani Dodoma (CPC) wapatikana. Wanahabari 42 walishiriki kutimiza wajibu wao muhimu wa kidemokrasia wa kuchagua viongozi. Uchaguzi ulisimamiwa na mwanasheria wa kujitegemea, ndugu Elias Machibya.

Joyce Kasiki ndiye mshindi wa uchaguzi kwa ngazi ya mwenyekiti aliyeshinda kwa kura 22 kati ya 42 dhidi ya mpinzani wake Christopher Mayeye aliyepata kura 20.

Israel Mgusi amefanikiwa kuwa katibu mkuu mpya wa CPC, kwa kushinda kwa kura 28 dhidi ya Abel Chidawali aliyepata kura 14.

Elias Machibya akifafanua jambo wakati wa uchaguzi.
Baadhi ya wanahabari walioshiriki kuchagua uongozi mpya
Uongozi uliopita wa chama cha waandishi wa habari Dodoma.
Ndugu Israel Mgusi (Katibu Mpya) akifafanua jambo baada ya uchaguzi
Bi. Joyce Kasiki (Kulia) akipokea mkono wa heko baada ya kushinda uchaguzi.