AJALI KATIKA MBIO ZA MWENGE DODOMA

MBIO za Mwenge wa Uhuru uliokuwa ukikimbizwa katika Wilaya ya Dodoma mjini zimeingia Dosari baada ya kupata ajali kilometa 3 kabla ya kukabidhiwa wiliya ya Mpwapwa.
Ajali hiyo iliyotokea jana majira ya 2;24 asubuhi katika mtelemko wa mlima fufu wilayani Chamwino na kusababisha watu 5 kujeruhiwa na kukimbizwa katika hospital ya mkoa ya General.
Watu hao ambao majina yao Bado hayajatambulika walipata majeraha katika maeneo mbali mbali ya miili yao ikiwemo kichwani, kifuani, mguuni na mikononi.
Kaimu Kamanda wa polisi Suzan Kaganda aliyefika na kujione hali ilivyokuwa katika eneo hilo alisema chanzo cha ajali hiyo ni Matuta yaliwekwa kwenye Barabara hiyo inayojengwa kwa kiwango cha lami toka fufu hadi Dodoma bila kuwa na alama yoyote.
Kaganda alisema baada ya Gali la polisi lililokuwa likiziongoza mbio hizo za mwenge pamoja na na lililokuwa limeubeba kupita ndipo ajali hiyo ikatokea baada ya gali ya nyuma kupanda moja yam awe yaliyokuwa kwenye matuta na kufunga Breki.
“Kutokana na vumbi jingi lililokuwa kwenye Barabara hiyo kutokana na msafara magali mengine, gali la nyuma lililigonga kwa nyuma na mengine yakafuata kiasi cha kufikia jumla ya magali 7 huku 5 yakishindwa kuendelea na msafara huo’’, alisema Kaganda
Aidha aliongeza kuwa msafara huo uliendelea na kukabidhiwa wilaya ya Mpwapwa tukio likifanywa na Lepphy Gembe wa Dodoma mjini na Chrstopher Kangoye wa Mpwapwa.
Mbio hizo za mwenge kitaifa ziliongozwa na Jama Ali Simai zenye ujumbe wa amani, Tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za Dini,itikadi, Rangi na Rasilimali