CHAMA CHA SKAUTI MKOA WA DODOMA WASHIRKI KATIKA SHUGHULI ZA JAMII

Maskauti wa Dodoma washiriki kwenye msiba na mazishi ya marehemu Florence Raphael. Bomalog iliwashududia vijana nadhifu na safi wa skauti wakiwa mstari wa mbele kutoa huduma kwa waombolezaji. Jambo hili limetiafaraja sana kwa wakazi wa Dodoma na kuweka ukaribu wa chama hicho na jamii inayowazunguka. Shughuli za msiba zilifanyika tarehe 31/07/2013 Iringa road karibu na shule ya Masingi Amani na mazishi yalifanyika siku hiyo kwenye makaburi ya Kikuyu karibu na chuo kikuu cha mtakatifu Yohana (St John's University).

Maskauti wakiwa mbele ya mwili wa marehemu wakati wa ibada

maskauti wakiwa tayari kuwahudumia waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa marehemu

Maskauti wakati wa kuhifadhi mwili wa marehemu

Pia Chama cha Skauti Wilaya ya Dodoma Mjini kimeandaa kambi ya kutwa (day camp) kwa wanachama wake. Kambi hiyo inatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 03/08/2013. Maskauti zaidi ya 150 wanatarajiwa kushiriki. Miongoni mwa mambo mengi yatayofanyika ni pamoja na Kupandisha Bendera kwa gwaride rasmi la Kiskauti na kuimaba wimbo wa TAZAMA RAMANI, zaidi shughuli za uhifadhi na usafi wa mazingira utafanyika. wadau wote wanakaribishwa.