KONGAMANO LA WANAWAKE KKKT-DODOMA

Wanawake wa kanisa la KKKT wa mkoani Dodoma kutoka wilaya za Dodoma mjini, Mpwapwa, Kondoa na kongwa, wameshiriki kwenye kongamano la wanawake wa kanisa hilo. Miongoni ya mengi yaliyofanyika ni kuchangia rasimu ya katiba, kujadili haki za watoto na maombi.

Kwa upande wa haki za watoto, washiriki wameiomba serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wavunjifu wa haki za watoto. Walipinga suala la kuwashirikisha watoto wadogo kwenye kupamba harusi (wasindikizaji) kwani hili linawaathiri kisaikolijia. Katibu wa idara ya wanawake na watoto amesisitiza kuhusu kuto elimu kwa jamii hasa ile ya malezi kwani kwa sasa taifa linakabiliwa na tatizo la mmomonyoka wa maadili.

BOMALOG inawapa heko wanawake wote wanaosimama imara kutetea mwelekeo chanya wa masuala ya kimaendeleo hasa haki za watoto. Zaidi mtoto umleavyo ndivyo akuavyo!

Katibu wa idara ya wanawake na watoto akizungumza jambo kwa washiriki

Mwinjilisti Daniel Kitua akiongoza maombi wakati wa kongamano.