MAONYESHO YA NANENANE 2013..

Maonyesho ya nanenane kitafa yanafanyika mkoani Dodoma. Wadau mbalimbali wanashiriki maonyesho hayo yaliyofunguliwa rasmi mnamo tarehe 01/08/2013 na kufikia kilele tarehe 08/08/2013.

Waziri wa kilimo chakula na ushirika Mh. Mhandisi Christopher Chiza alitembelea viwanja vya nanenane vilivyo maeneo ya Nzuguni kwenye manispaa ya Dodoma. BOMALOG ilimmulika kama aonekanvyo:

NI NGOMA YA KUMKARIBISHA MHESHIMIWA HIYO! WE ACHA TU!
MH. WAZIRI (KUSHOTO) AKIPTA MAELEZO TOKA KWA MSHIRIKI WA MAONYESHO
HUU ULIKUWA NI UFAFANUZI MURUA JUU YA MBEGU ZA ALIZETI
PAMBA NI ZAO LILISHIRIKI MAONYESHO! NA WAZIRI AMELIONA! YAANI NI NZURI..
"HILI NI BILINGANYA LA KITAIFA! NI KUBWA KAMA BOGA. UKIONA BOGA LENYEWE?"
MAKAMANDA WA MAGEREZA WAPO MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA TAIFA HALIHISI NJAA! SAFI SANA!