MOTIVATIONAL MOMENT AT MLIMWA SECONDARY SCHOOL

CHANGE MINDS CHANGE LIVES (cmcl) taasisi inayojihusisha na uhamasishaji wa masuala ya maendeleo miongoni mwa vijana, imefanya semina fupi juu ya umuhimu na namna ya kusoma vitabu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mlimwa iliyo kwenye manispaa ya Dodoma.

Semina hiyo iliandaliwa kwa ushirikiano wa CMCL na BOMALOG. Washiriki walipata wasaa wa kujifunza vingi na kuelewa umuhimu wa kusoma vitabu. Zaidi waalimu wa shule hiyo wameahidi kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha program za kusoma vitabu kwa muda wa ziada zinatekelezwa mara moja.

BOMALOG inawaalika wadau wa maendeleo kushirikiana nasi katika kufanikisha malengo hususan ya kuifikia jamii kwa 100% . Na kushiriki kikamilifu katika shughuli za elimu kwa vijana hasa kupitia kipengele cha TEENS CLUB ambacho huwashirikisha vijana kwenye maeneo yao na shule yao.

Shemeji Melayeki, amekuwa msitari wa mbele kuona vijana wanapata ufunguzi wa kimtazamo na fikra (change of mind set) kwa kuwafikia vijana kwa hali na mali. kumbuka ni wakati wako kwa jamii yako.....JIUNGE NASI!

WANAFUNZI WAKIWA MAKINI KWENYE SEMINA

SHEMEJI MELAYEKI AKISISITIZA JAMBO KWA WANAFUNZI

KWA KWELI NI MOTIVATIONAL MOMENT

UFAFANUZI ZAIDI ULIHITAJIKA BAADA YA SEMINA. SHEMEJI AKIELEKEZA JAMBO KWA WANAFUNZI

SHULE NZIMA ILIKUWA MAKINI NI HAMASA YA UHAKIKA