UJENZI WA VIBANDA STENDI YA JAMATINI DODOMA WASIMAMISHWAMWENYEKITI wa kamati ya Mipango miji na Mazingira Manisipaa ya Dodoma Stephen Mwanga Amesimamisha ujenzi wa vibanda vya wafanya Biashara ndogondogo [machinga] katika stend ya Daladala ya Jamatini baada ya kutolidhishwa na Ugawaji wa nafasi zao.

Machinga hao wamesimamishwa kujenga siku ya kwanza tangu stend hiyo kuanza kutumika baada ya kufungwa mwaka mmoja uliopita ili kupisha ujenzi utakaokidhi haja ya watumiaji wa magali hayo yanayotoa huduma za usafiri wa ndani ya mji huo.

Mwenyekiti huyo aliwataka kusimamisha zoezi hilo la ujengaji wa vibanda vya biashara zao kutokana na kile alichosema ugawaji ugawaji wa nafasi hauzingitia utarabu kutokana na viongozi wa machinga hao kupewa jukumu la kusimamia.

Mwanga aliongeza kuwa alifika eneo hilo kutokana na kusikia malalamiko ya baadhi ya machinga kulalakia kutotendewa haki wakati zoezi la ugawaji likiendelea kwakuwa wengi wao walijikuta wakiwekwa pembeni tofauti na walipokuwa kabla ujenzi huo haujaanza Augost 2012.

Alisema alipofika na kujionea kilichokuwa kikiendelea Stend hapo aliamua kumjulisha mkurugenzi hali halisi na hivyo kuamuliwa zoezi la ujenzi na uwekaji wa vibanda lisimamishwe na kamati ndogo iundwe ili ikutane na uongozi wa manispaa ili walijadili na kuliweka sawa swala hilo.

'' Nimesimamisha ujezi usiendelee kwa sababu mtu akishajenga kumuondoa inakuwa ngumu, mimi na kamati yangu ya mipango miji na mazingira tutakutana na Meya na Mkurugenzi wa manispaa ili tulitatue swala hili kwa pamoja na kamati yao mapema iwezekanavyo ili Abiria waendele kupata mahitaji yao kama kawaida'', alisema Mwanga

kwa upande wao baadhi ya Machinga hao walisema viongozi wamejilimbikizia nafasi zaidi ya moja kwa kutumia majina tofauti mpaka ya wake zao huku sura nyingi mpya zikipenyezwa hata wakati staend hiyo kabla ya kuhamishwa hawakuwepo huku nafasi hizo zikibanwa kuwa ndogo na wao kujipendelea nafasi za mwanzo.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao wadogo wadogo Haji kulaya alisema mpangilio huo wa viongozi hauwezi kubadilishwa kutokana na ramani ya stand hiyo kubadilika kuwa tofauti na ilivyokuwa mwanzo hali iliyofanya kuwe na mpangilio mpya katika ugawaji.

majina yakisomwa

uvunjaji wa mabanda

nahama na banda langu