USHIRIKINA VS SHERIA MIKONONI

Diwani wa viti maalumu kata ya Chalinze, mh. Mary Mazengo, amethibitisha kutokea kwa mauaji ya kikatili ya mwalimu wa shule ya msingi Manchali, Leah Goden (50). Mwalimu huyo aliuawa kikatili na wananchi wenye hasira kali kwa kumtuhumu kufanya ushirikina.

Mwalimu huyo alihusishwa na matukio ya vifo vya watu wanne wakiwemo watoto wake wawili, mpenzi wake na mwalimu mkuu wa shule hiyo kwa kipindi cha miaka milwili.

Kutokana na kuuawa kwa mwalimu Leah, wananchi wamekesha wakifurahi na kunywa pombe kwani hofu yao juu ya kudhuriwa na mwalimu huyo kwa sumu ama uchawi kama alivyotuhumiwa kusababisha vifo vya mpenzi wake na mwalimu mkuu haipo tena.

Kutokana na tukio hili BOMALOG inaungana na Mh. Diwani, Mary Mazengo kuwasihi wananchi kutojichukulia sheria mikononi, na badala yake kufuata na kuzingatia utawala wa sheria na kujiepusha na imani potofu ambazo ni kichocheo kikubwa cha migogoro katika jamii.