WAKAZI WA DODOMA WALALAMIKIA UDOGO WA STENDI MPYA YA DALADALA

WAKAZI wa manispaa ya Dodoma wamelalamikia udogo wa Stand kuu ya Daladala ya Jamatini na kuitaka mamlaka nayohusika kuliacha eneo la oil com zilikokuwa zikipakilia abiria wakati wa ujenzi wa stand hiyo kuwa mbadala kutokana na wingi wa magali.

Kauli hiyo ilitolewa wakati stendi hiyo ilipoanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza jana ambapo ilishuhudiwa wingi wa magali hayo ya Abaria yakiingia na kutoka huku kukiwa na msongamano mkuwa kiasi cha mengine kushushia abiria Barabarani.

Mmoja wa Abiria wanaotumia stand hiyo Winnie Binamu alisema imejengwa vizuri lakini haikidhi haja kutokana na kuwa ndogo ukilinganisha na idadi kubwa ya Daladala zilizopo hali inayosababisha msongamano na wengi kushusha abiria bila utaratibu ilimradi wawahi kupakia wengine.


Winnie aliongeza kuwa niafadhali kama wahusika wangeiacha stand iliyokuwa ikitumika kwa muda ya oili com kuendelea kutumiwa na baadhi ya magali ya njia nyingine na mengine kupelekwa jamatini kwa sababu kwa sasa watu ni wengi tofauti na miaka ya nyuma.

Kwa upande wao madereva wa Daladala hizi walisema stand pamoja na uzuri haikidha kutokana na njia moja kuwa na magali zaidi ya 50 wakitolea mfano njia ya Chang'ombe, Mipango, UDOM, na kisasa zenye abiria na Magali Mengi.

Mmoja wa madereva wa Daladala zinazoelekea Ipagala Moses Mamba alisema kwa sasa Dodoma inawatu Wengi walioletelezwa na vyuo pamaja na taasisi zilizo na zisizo za kiserekali zinazoendelea kuhamia mkoani hapa hivyo ni vyema swala la stand hiyo kuangaliwa upya na ikibidi iwekwe ya ziada.

'' Ona ndugu mwandishi leo ni siku ya kwanza stand hii kuanza kutumika lakini msongamano ni kama unavyoona wengi wanashushia abaria barabarani kuanzia hapa yanapoingilia maka karibu na kipita shoto[ Round About] cha stand ya mabasi ya mkoani je wakija wote kutokana na tunavyojua itakuwaje?'', Alihoji Mamba

Katibu wa Umoja wa wenye Daladala [UWEDO] Peter Kabome alisema Stendi hiyo haijawa Rasmi ni kama inafanyiwa majaribio kwa sababu haiwezekanai yakatakiwa kuingizwa magali zaidi ya 300 kwenye eneo linalochukua magali yasiyozidi 100.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira manispaa Stephen Mwanga alisema ameona msongamano huo jinsi ulivyo mkubwa hivyo atahakikisha anavihusisha vyombo vinavyohusika kikiwemo SAMATRA ili waweze kuona nini cha kufanya ili walau kuliweka sawa la staend hiyo.
msongamano katika stand mpya ya jamatini

hali ilivyo katika stand mpya ya jamatini

tinga tinga likibomoa stand iliyokuwa ikitumika kwa muda