ATUPA KICHANGA

JESHI la polisi mkaoani Dodoma linamshikilia Mwanamke mmoja kwa kosa la kumtumbukiza mtoto chooni akiwa hospatali ya mkoa alikopelekwa kujifungua.
Tukio la kukamatwa kwa mwanamke huyo aliyekuwa amepelekwa katika hospital ya Rufaa yamkoani hapa baada ya kushikwa na uchungu wa kujifungua lilitokea majira ya saa tisa usiku.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Damas Nyanda Alimtaja mwanamke huyo kuwa anaitwa Sinsia Laurent 28 msandawe mkazi wa uhindini mjini hapa.
Nyanda alisema baada ya kufikishwa hospitalini aliomba kwenda chooni kujisaidia na baadae manesi wabaini kulikuwa na mwili wa kichanga muda mfupi baada  ya mtuhumiwa huyo kutoka chooni.
‘’tulipokea taarifa muda huo na tulipofika tulikuta mwili wa kichanga cha jinsia ya kiume ukiwa nje wakati kichwa kikiwa tayali kimesukumwa ndani ya choo hicho tulipomtoa alikuwa tayali ameshafariki’’, alisema Nyanda.
Aidha nyanda alisema wanaendelea kumshikilia mwanamke huyo  na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.    
Kwa upande wake Leah aliyempeleka hospilini hapo ambae mfanyakazi mwenzie katika baa ya CDA Club iliyopo Uhindini alisema mtuhumiwa huyo siyo mkweli kwa kutoweka wazi kuwa mimba yake ilikuwa na miezi mingapi maana wao waliambiwa ilikuwa na miezi 5.
Aliongeza kuwa kitendo hicho alichokifanya Mwenzao ni cha kinyama na hakistahili kufanywa katika nyakati tulizonazo maana kuna njia nyingi za kuzuia mimba kama anakuwa hayuko tayali kupata mtoto