MSIKITI CHUPUCHUPU KUTEKETEA

Moto mkubwa umezuka katika msikiti wa manyema uliopo barabara ya saba manispaa ya Dodoma na kusababisha uaharibifu wa sehemu ya jingo hilo pamoja na samani mbalimbali.
Mashuhuda wa Tukio hilo waliambia BOMALOG RADIO kuwa baada ya kuswali swala ya ijumaa na kuondoka walishtukia moshi mkubwa ukisambaa kutokea juu ya msikiti huo.
Walisema baada ya kuona hivyo waliamua kuwajulisha kikosi cha zimamoto kwa kutumia simu zao na baada ya muda mfupi walifika na kuanza kuzima Moto huo uliokuwa ukisambaa kwa kasi kuanzia juu ya ghorofa ya msikiti huo.
Mmoja waumini hao alietambulika kwa jina moja la Said alisema waliona moto huo ukianzia juu  kwenye maungio ya umeme sehehemu ya main switch ambapo uliendelea kusambaa kabla ya kudhibitiwa na kikosi cha zimamoto.
Kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Dodoma Damas Nyanda aliyefika na kujionea hali halisi alisema walikuwa bado hawajapata taarifa kama kulikuwa na mtu yeyete aliyejeruhiwa ama kupoteza maisha.
Alisema mpaka wakiti huo walikuwa wanaendele na zoezi la uokoaji na baada ya mambo yate kuhakikiwa taarifa rasmi ya hasa iliyopatikana baada ya tahimini ya viongozi wa msikiti huo.
Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha zimamoto mkoa Sajenti Amiry Issa alisema walifika Dakika 4 baada ya kupokea Taarifa ya ajali hiyo ya Moto na kukuta moto umesamba maeneo mbalimbali ya msikiti huo wenye ghorofa moja.
Issa alisema urahisi wa kuzima moto huo ulitokana na wao kupewa taarifa mapema kabla ya moto kusambaa sana na kuwa na madhara makubwa.
Akatumia fursa hiyo kuwataka watu kutofanya juhudi za kuzima moto wowote unaojitokeza wenyewe kabla ya kuwajulisha zimamoto, maana kwa kufanya hivyo kunachelewesha uzimaji na kusababisha hasara kubwa
BOMALOG RADIO ilishuhudia Mazuria yanayotumiwa kuswali, vitabu, kanzu na nafaka iliyokuwa ghorofa ya juu kuwa imeunguzwa na moto huo uliozuka kuanzia majira ya saa 8. 10 mchana.