TAMBIKO LA KIMILA NA LALAMIKO LA MAWASILIANO

2 FUNDI NA MKEWE.JPG


WAKAZI wa kata ya Segara Wilayani Chamwino mkoani Dodoma wamelalamikia kukosekana kwa huduma ya mawasiliano hali inayowafanya kukosa huduma za msingi kwa wakati ikiwemo kuuza mazao kwa bei yahasara.

Wakazi hao waliitoa kauli hiyo katika kijiji cha Malechala walipokuwa kwenye Tambiko la kimila lilihudhuliwa na makabila mbalimbali yaliyoongozwa na Wanguu toka mkoani Tanga lililohudhuriwa na watu zaidi ya 400 na kufanyika katika himaya ya Fundi  Shabani Waziri  mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho Asha Mohamed   alisema kumekuwa na kelo ya ukosefu wa mitandao ya mawasiliano tangu ilipoanzishwa hapa nchini hali ambayo imekuwa ikiwasababishia kukosa kila huduma za kijamii kwa wakati.

Alisema kutokana na kata hiyo kuwa mbali na makao makuu ya wilaya hiyo ya Chamwino wamekuwa wakipata taabu ya utoaji wa taarifa za matukio mbalimbali zikiwemo za ajali, ujambazi, wizi, wagonjwa wanaohitaji huduma za haraka pia wameshindwa kujua wakati mzuri bei za mazao.

Asha aliongeza kuwa katika vijiji vya Dabalo, Izava, Chiwondo, Mapange, Magungu na ikombo vinavyojishughulisha na kilimo cha Ufuta, Karanga, Alizeti na Mahindi kwa ajili ya biashara ambayo wamekua wakisafirisha kupeleka Dodoma na Arusha kufuata japo mara nyingi wamekuwa wakikuta bei zipo chini kutokana na kuondoka bila mawiliano.

“Tumekuwa tukipata taabu sana hasa tunaposafirisha mazao mara nyingi tumekuta bei zipo chini kutokana na ukosefu wa mawasiliano, kama tungekuwa na mawasiliano tungejua mapema kama zipo chini na ingekuwa hiyali mtu kusafirisha,

Hapa tulipo unaona mlima ulee km 1  ndipo pana mawasiliano tena ya mang’amng’am maana ukipata hutakiwi hata kugeuka maana yanakata, usiku umelala linatokea jambo huwezi kupiga simu ndani mpaka ufike kule hivi kweli viongozi hawaoni au wao kwa sababu hawaishi huku vijijini?’’, alihoji Asha

Aidha alisema wakazi wote wa kata hiyo wanapotoka nje ya kata hiyo ndipo huonja radha ya mawasiliano bila bugudha kwani pamoja na wengi wao kuwa na simu tena za gharama wamezigeuza kuwa radio kaaseti za kuchezea na kusikilizia miziki.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Malecela Nganiki Sailepu alisema Ukosefu wa mitandao ya mawasiliano kwa njia ya simu limeigharimu kata hiyo kwa kipindi kilefu, ambapo pamoja na juhudi za kumfikishia Mbunge wao wa jimbo la chilonwa Hezekiah Chibulunje na viongozi wa Wilaya hiyo wamishia ahadi zisizotekelezwa.

Sailepu alisema kuanzia wapewe ahadi hiyo mpaka sasa ni zaidi ya miaka 4 hakuna lolote ambalo limefanyika badala yake wamekuwa wakipigwa Danadana na kila kiongozi wa wilaya anayekanyaga kata hiyo ambayo inategemewa kwa kiwango kikubwa kwa kilimo cha mazao ya Chakula na Biashara mkoni Dodoma.
7 Ngoma.JPG
Waganga hao wakiche moja ya ngoma za Kinguu wakati walipokuwa wakijiandaa kuanza tambiko rasmi
Tambiko hilo lilihudhuriwa na viongozi  mbalimbali wa kijadi na wakiserekali lilijumuisha waganga zaidi ya 800 wanaojihusisha na Tiba za jadi waliotoka mikoa ya Dodoma, Tanga na Kagera, waliofika kujinoa zaidi ambapo Mgeni Rasmi alikuwa kiongozi wa kimila wa kabila la kinguu Fundi mkuu Sangali Chambo.
1 ngoma mtini.JPG
Waganga wa Tiba za jadi na Ukunga wakiongozwa kuimba na kucheza Ngoma aina ya Ng'anga ambayo huchezwa juu ya kilingo kama ishara ya kupandishwa vyeo walipokuwa wakimalizia Tambiko la kijadi lilifanyika kwenye himaya ya Shabani Waziri, lililofanyika kijiji cha malecela wilayani Chamwino.
4 MIKONO TUNGULI.JPG
WAGANGA NA TUNGULI