WANAOFADHILIWA NA HURUMA WAACHE UTORO

WAZAZI wametakiwa kuwahimiza watoto wao kuzingatia masomo katika shule wanazosoma ili waweze kuwa msaada katika maisha yao ya baadae.
Kauri hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa mtaa wa mathias miyuji katika manispaa ya Dodoma Edward Lenjima alipokuwa akiongea na wazazi wa wanafunzi wanaofadhiliwa na shirika la Huruma Women Goroup la mjini hapa.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa imekuwa ni kawaida ya wazazi wengi kutozingatia ipasavyo kuhusu maendeleo ya watoto wao kiasi cha watoto hao kuwa watoro mashuleni.
Lenjima alisema ni vizuri wazazi kujua umuhim wa watoto wao kuzingatia masomo kwa sababu baadae watakuwa msaada kwa wazazi wao pindi watakapokuwa na kazi za kuajiliwa na kujiajili zatakazotona na Elimu.
‘’Mimi kama mwenyekiti sitaki mzazi yoyote kuzembea swala la Elimu kwa mtoto wake kwani wazazi wengi hawana uwezo wa kumudu masomo ya watoto wao hivyo kama Huruma wamejitolea kuwafadhili ni vyema kuthamini kwa kuwahimiza kusoma’’, alisema Lenjima
Kwa upande wao wazazi hao waliahidi kuwahimiza watoto wao kuzingatia Elimu lakini pia kuwashukuru shirika hilo la huruma kwa kutokana namisaada ya mara kwa mara kwenye eneo hilo la elimu kwa vijana wao.
Nae Mhasibu wa Shirika hilo la Huruma women Group linalowezeshwa na SATF ya jijini Dar es laam Azgard Muhembano alisema wamekuwa wakitoa ufadhili wa Ada na vifaa vya kusomea kwa wanafunzi wa Msingi na Sekondari na tangu wameanza wanajivunia watano waliopo vyuo vikuu.   
Aliongeza kuwa wanahudumia jumla ya wanafunzi wa shule za msingi 39 na wa sekondari 36 wa hombolo, makutupola na miyuji ambapo waligawa vifaa vya kusomea na sale za shule vya 7.9 mil.