UONGOZI WA MACHINGA WAPINGWA CHINI

WAFANYABIASHARA ndogondogo maarufu kama machinga wa stendi ya daladala jamatini mjini Dodoma wameukataa uongozi wao wa muda kutokana na Tuhuma mbalimbali ikiwemo ufujaji fedha.
Wafanyabiashara hao walifikia hatua hiyo Kwenye mkutano wao maalumu waliouitisha wenyewe juzi kwa lengo la kuwataka viongozi wao hao wa muda wawafafanulie mambo mbalimbali yakiwemo ya kutoitisha mkutano mkuu wa uchaguzi.
Akiongea kwenye mkutano huo Katibu wa Muda wa kamati teule Sylvester Pius  aliyeteuliwa baada ya kusubili saa nzima bila viongozi wao kutofika pamoja na kupewa barua ya kuitwa kwenye mkutano huo alisema tangu juni 2010 Uchaguzi mkuu haujafanyika.
Alisema tangu mwaka huo machinga hao bado hawana katiba hali inayowawia vigumu hata kusajili umoja wao ili uweze kutambulika, Kutokan na kukosekana kwa mikutano hata mapato na matumizi hayasomwi, kumekuwa na fedha za viingilio na ada 3000, michango mingine ya vitamburisho elfu 20, elfu 1500 za kadi za CCM na 2000 ya barua ya utamburisho manispaa kwa kila  kwa ajili ya kusaini mikataba kwa wanachama zaidi ya wanachama 80.
Pius aliongeza kuwa kutokana na tuhuma hizo kuna haja ya kuchukua hatua za makusudi ili walau kuufanya umoja huo uweze kuwa na manufaa kwa wanachama badala ya kuwaachaia viongozi hao wa muda ambao wameshindwa hata kujulisha wanachama wao wanachoingiza na kutoa kwa kipindi chate cha miaka4 badala yake wamegeuka kuwa wababe.
‘’Hakuna haja ya kuendelea na viongozi wa muda tena tuhakikishe tunateua kamati ambayo pamoja na mambo mengine inaandaa mkutano mkuu wa uchaguzi mapema iwezekanavyo na kamati hiyo itambulishwe kwa wadau wa stendi hiyo ili waweze kufanya kazi zetu kiurahisi bila vikwazo’’
‘’Vilevile kamati hiyo ifuatilie nyaraka zote za umoja kwa waliokuwa viongozi wa muda ili ziwaongoze kufanya kazi na kwa kuwa umoja ni nguvu na utengano ni zaifu tushilikiane kwa pamoja’’, alisema Pius
Baadhi David Magere alisema uogozi wa muda ulikuwa unajali sana masrhi yao na si kufanya kazi za umoja kwa ufanisi ndiyo sababu hata miongoni mwawanaumoja wanapopata matatizi uongozi huo ulikuwa unaangalia tuu bila kusema kufanya lolote, katiba iwe ni jambo la kwanza ili tutakaowachagua waongeze kwa kufuata sheria.
Kwa upande wake Katibu wa Muda aliyesimamishwa Sospeter Chagonela alisema wao hawawezi kuacha uongozi hata kama wanaumoja wameteua kamati nyingine kwa sababu wao wamekasmiwa madaraka na manispaa hivyo wao ndiyo watakaochagua viongozi na kuwajulisha manispaa kwa Barua kuwa hao ndio viongozi wakufanya nao kazi na si vinginevyo.
Umoja huo ulianzishwa Juni 2010 kwa lengo la kushikamana na kusaidina katika maswala ya kijamii na kiuchumi ukianza na jumla ya wanachama 18 na baadaekuongezeka na kufikia 41 kabla ya orodha ndefu iliyoandikwa na uongozi wa muda kutokana na machinga hao kutakiwa kupisha ujenzi wa stendi hiyo ambayo kwa sasa imekamilika na kuanza kutumiaka takribani mwezi mmoja sasa