UZINDUZI WA POLISI TARAFA ( ZONE TASK FORCE)

PIKIPIKI zinazotolewa kwa jeshi la polisi mkoani Dodoma na wahsani mbalimbali ni kwa ajili ya kuwahi matukio hazitolewi kwa ajili ya matumizi ya nyumba ndogo za askari.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Lephy Gembe alipokuwa akizindua  Mradi wa polisi Jamii unaojulikana kama ZONE TASK FORCE  iliyohusisha mjini, Zuzu na kikombo
Mkuu huyo wa wilaya alisema pikipiki hizo zinatolewa kwa lengo maarumu la kuwahi kwenye matukio pondi polisi wanapopata taarifa ya uhalifu unafanyika au unaopangwa kufanyika mahali na si za kutembelea au kuendea kwenye nyumba ndogo.
Aidha Gembe alisema vikosi kazi vya tarafa [TASK FORCE] ,ambavyo lengo lake kuu ni kuendeleza na kusimamia shughuli za ulinzi na usalama wa tarafa hizo  kwa kuzingatia sera ya ushirikishwaji  wa jamii
Aliongeza kuwa mpang o huo wa uzinduzi wa tarafa , vikosi kazi pamoja na shughuli za polisi jamii ni kuhakikisha kuwa makosa yanayoweza kujitokeza katika tarafa ambayo yanaweza kuwafanya wananchi wetu wasifanye mambo ya maendeleo yao kiufanisi yanaondolewa kabisa katika jamii.
Awali akizungumza kwenye uzinduzi huo kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Damas Nyanda alisema lengo kuu la uzinduzi huo ni katika kuendeleza, kuimalisha ulinzi  na usalama nchini, katika kutekeleza mpango mkakati wa kuweka askari wasiopungua 15 kwa kila Tarafa.
Katika uzinduzi huo ambao jeshi hilo lilikabidhiwa pikipiki tatu zilizotolewa na Benk ya NMB na moja kamanda wa jeshi hilo David Miseme, huku mdau mwingine wa ulinzi shirikishi Diwani wa kata ya Tambukareli Adamu Perugina alikabidhi mizinga 50 kwaajili ya ufugaji wa nyuki  kwa ajili ya vijana kiuchumi wanaoendelea  na polisi jamii.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Lephy Gembe akiendesha moja ya pikipiki zilizotolewa na Benki ya NMB ili kuchangia hatua za serikali za kuhakikisha jeshi la polisi linakuwa na usafiri wa uhakika kwa ajiliya matukio ya uhalifu kwenye uzinduzi wa ulinzi shirikishi tarafa.


               
Vijana walihamasika na kujiunga na ulinzi shilikishi waonyesha namna ya kupambana na waharifu pindi wanapokumbana uso kwa uso wakati wa uzinduzi wa polisi jamii kwa tarafa ya mjini iliyozihusisha kata za hombolo, kikombo, zuzu

Mkuu wa polisi Wilaya ya Dodoma Mjini Tadei Malingum akiwaonyesha viongozi wa serekali wilaya ya Dodoma mjini Pikipiki 3 zilizotolewa  na wadau wa polisi jamii ikiwemo Benki ya NMB kwa ajili ya ulinzi shirikisha Tarafa ya manispaa
Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Lephy Gembe akimkabidhi polisi tarafa polisi tarafa George Andala moja ya mizinga 50  iliyotolewa na mdau wa polisi jamii Diwani wa kata ya Tambukareli Adamu Perugina kwa ajili ya kuinua uchumi wa kitengo hicho cha ulinzi shirikishi