UZINDUZI WA TAWI JIPYA LA CCM CHANG'OMBE MAGHARIBI

Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma Albart Mgumba akikata utepe kuzindua ofisi za chama hicho kata ya  Chang'mbe iliyopo chang'mbe Magharibi
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Drt David Malole akiwa na viongozi wa CCM kata ya Chang'mbe walipokuwa wakimsubiri Mgeni Rasmi kwa ajili ya kuzindua ofisi ya chama hicho kata ya Chang'ombe na baadae kuwahutubia wananchi.

Katibu wa CCM Mkoa Albart Mgumba akimtambulimbulisha Katibu wa umoja wa wanawake wa chama hicho [UWT] Kaundime Kasasi ambaye pia ni Bibi Mzazi wa Miss Tanzania 2013 Happyness Watimanywa kwa wananchi wa kata ya Chang'ombe, kabla ya kuwahutubia wananchi hao.

Diwani wa Kata ya Chang'mbe Bakari Fundikira mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kutokea Katika manispaa ya Dodoma akiwa kwenye Pikipiki ya mataili matatu maarufu kama bajaj yenye mashine yenye dawa ya kuulia mazalia ya mbu ambayo wameikabidhiwa miezi 2 iliyopita baada ya kukwama kusikojulikana baada ya kutolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Tangu mwaka 2011 kabla ya yeye kuwa Diwani 

Jengo la ofisi ya CCM linavyoonekana baada ya kukamilika kwaajili ya matumizi kama linavyoonekana.

Wananchi wakiwa eneo la mkutano mkutano wakisubiri kuhutubiwa na katibu wa ccm mkoa.katibu akisalimiana na Wananchi