WANAFUNZI WAWILI CBE WAPOTEZA MAISHA

Asikari wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa barabara
sehemu ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la mizigo.
WANAFUNZI wawili wa chuo cha biashara (CBE ) wamepoteza maisha papo hapo kwenye ajali baada ya kugonga tela la mizigo lililokwama barabarani baada ya kuharibika. Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya kugonga tela la lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa wakitokea kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika kijiji cha ihumwa manispaa ya Dodoma. Bomalog ilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo iliyopo pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa takribani saa zaidi ya tatu kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika na kuongoza utaratibu wa kuondoka. Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa wanafunzi hao wakati wakiendesha pikipiki hiyo yenye namba za usajili T 420 CCN waliokuwa wakukitokea barabara ya morogoro kuingia mjini. Suzan aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala wanafunzi wa CBE na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 477 ABM na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya wiki bala kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara hiyo yakiendelea katik eneo hilo. Aliongeza kuwa miili ya marehemu hao iliyokuwa imehalibika vibaya kutokana na kufumuka fuvu la kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo na ubongo kusambaa katika eneo hilo imehifadhiwa katika hospital ya mkoa.

Baadhi ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa
msaada katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha
biashara CBE Dodoma.
Miili ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya
kuondolewa katika kijiji cha ihumwa barabara ya morogoro Dodoma kabla
ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.


.Baadhi ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma  waliokufa
kutokana na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi

huku lori hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote
barabarani hapo