INAWEZEKANA KUSEMA BAAAAASI KWA VITENDO!

MCHUMI wa manispaa ya Dodoma Isaack Kissa amefukuzwa kazi kutokana na
ubadhilifu wa Fedha zaidi million 60 alizotafuna.Maamuzi hayo yalitolewa kwenye mkutano wa Baraza maalum la madiwani lilokutana kutolea maamuzi swala hilo lilodumu zaidi ya mwaka.

Mstahiki meya wa manispaa hiyo Emanuel Mwiliko alisema fedha hizo zilizofujwa na mchumi huyo zilitumika zaidi ya zilivyoidhinishwa na bodi ya zabuni ya halmashauri ya manispaa hiyo. Alisema Kissa alishiriki kufanya malipo ya shs 154, 565,250 badala ya 94,130,400 sawa na yen za kijapani4, 800,000 yaliyoidhinishwa na bodi ya zabuni ya halmashauri mei 21, 2012.

Aliongeza kuwa kiasi hicho cha fedha kilichotumiwa kununulia gari aina ya Nissan Station Wagon lenye namba za usajili SM 9820 kwa ajili ya matumizi ya halmashauri hiyo kilikuwa na ongezeko la 60,434,850 ambazo ndizo ziliibwa. ‘’Uamuzi wa kufukuzwa kazi ndugu Kissa umetolewa baada ya kubainika ametumia vibaya fhedha za manispaa, maamuzi hayo yakitolewa na Madiwani baada ya majadiliano ya wajumbe wa vyama waliokubaliana kufukuzwa kazi Mchumi huyo’’,alisema Mwiliko.

Aidha watendaji wa mitaa Stella Kigosi  na Emakali hayo ya Madiwani Eunice Goliama wamebadilishiwa vituo vya kazi kutokana na utendaji usioridhisha kutokana na makusa mbalimbali huku wakionywa kuwa kwenye uangalizi.

Meya huyo aliwataka watumishi wote wa Halmashauri kuhakikisha
wanafanya kazi kwa kufuata maadili na kujiepusha na tamaa huku akionya kuwa kama hawatakuwa waangalifu wajue ipo siku watavuna walichopanda hata kama kwa kuchelewa.