WANAFUNZI WAASWA KUACHA NGONO

WASICHANA wasomi wa vyuo vikuu wametakiwa kujiepusha na uhuni wa
kingono na badala yake wazingatie malengo yaliyowapeleka masomoni ili
kuepuka kuzitia hasara familia zao na taifa kwa ujumla
Haya yalisemwa na Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Salma Kikwete alipokuwa
azindua Kongamano la wanafunzi wasichana wa Vyuo vikuu lilofanyika
Chuo kikuu cha Dodoma [UDOM]
Salma alisema kumekuwa na tabia ya wasichana wa vyuo vya elimu ya juu
kuwa na wanaume watatu kwa wakati mmoja ambao wao huwaita moja wa
pamba yaani mavazi, mwengine ni wa kumsaidia darasani kimasomo na
mwingine wa ukweli yaani anayempenda huku wakijidanganya kuwachuna na
kumbe wanachunwa wao kutokana na kila mtu kuwa na nguvu yake wakati wa
tendo
 Salma alisema wasichana hao wanatakiwa kujua wapo masomoni kwa
malengo maarumu ya kuzisaidia familia, jamii zinazowazunguka na taifa
kwa ujumla mara baada ya kumaliza masomo yao hivyo wanatakiwa
kujiepusha na starehe zisizo maana zinazotokana na kujirahsisha.
Mke huyo wa Rais mwenye fani ya ualimu aliwataka wasichana hao
kuhakikisha wanajitambua kama ni wanawake wenye maumbile tofauti na
wanaume  na hivyo kuhakikisha wanaiweka miili yao kuwa katika uthamini
mara baada ya kuvunja ungo kinyume cha hapo ni mimba na magonjwa ya
ngono.
Aliwafananisha wasichana na madini aina ya Lulu yanayopatikana ndani
ya samaki chaza anaishi miambani kwenye kina kilefu cha bahari na
hivyo kutokana na ugumu wa upatikananaji wake mara nyingi ilikuwa
ikitumiwa na wake wa wafalme  pekee.
''Wasichana zitunzeni Lulu zenu kwaajili ya manufaa yenu ya baadae
acheni tabia za  kujihusisha na ngono, ni lazima mjua kwamba familia
zimejifunga mkanda kukusomesheni ili mje kuzisaidia hivyo wanaume
mliokutana nao vyuoni mjue kabisa sio hao watakao kuwa wenzi wenu
katika maisha wanawapotezea muda wa masomo bure'', alisema
Aidha Mama Kikwete Aliwaambia wasomi hao wa kike wa vyuo vikuu kuwa
wanatakiwa kuwa na tabia njema ambayo itawafanya wapate mafanikio
katika kila Nyanja watakazopitia na hatimae kuwa viongozi wazuri wa
familia na taifa hili.
Salma alizindua Kongamano hilo lililoandaliwa na Wanafunzi wa chuo
Kikuu cha Dodoma lilivikutanisha vyuo vikuu vya Serikali za Mitaa,
Madini, Mtakatifu Yohana, CBE na Mzumbe walikuwepo Dodoma kutembelea
Bunge la bajeti na wiki ijayo anatarajia kuzindua mpango wa upimaji na
matibabu ya salatani ya shingo ya uzazi kwa wanawake Wilayani Bahi
leo.