Magufuli amteua Majaliwa kuwa waziri mkuuRaisi wa Tanzania John Magufuli amempendekeza mbunge wa Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa awe waziri mkuu mpya. Tangazo la uteuzi wa Bw Majaliwa limetolewa bungeni na Spika Job Ndugai. Bunge limeahirishwa kwa dakika 45 kuwapa muda wabunge kuchambua uteuzi huo kabla ya kurejea na kupiga kura. Bw Majaliwa amekuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa, Jimbo la Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) tangu 2010.Eneo la Ruangwa linapatikana kusini mashariki mwa Tanzania. Alikuwa naibu waziri katika afisi ya Waziri Mkuu aliyehusika na utawala wa mikoa na serikali za mitaa katika serikali ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete. Alihudumu pia kama naibu waziri wa elimu.