MAGUFULI AMWAPISHA MIGIRO


Hafla ya kuapishwa kwa Dk Asha-Rose Migiro imefanyika  katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Dodoma. Rais John Magufuli amemuapisha Dk Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Hafla ya kuapishwa kwa Dk Asha-Rose Migiro imefanyika leo  katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Asha-Rose Migiro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kallaghe ambaye amerudishwa nyumbani.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Dk Migiro ameahidi utumishi uliotukuka na kwamba atahakikisha uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Uingereza unaimarishwa zaidi, hususani katika kuvutia uwekezaji, biashara na utalii baina ya nchi hizi mbili.

Migiro pia ametoa wito kwa watanzania waliopo hapa nchini na waishio Uingereza kuitumia ofisi hiyo ya ubalozi ipasavyo, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali hasa za kiuchumi.