SABABU ZA KUMILIKI TECNO BOOM J8 ZATAJWAmambo mengi sana lakini hapa yapo matano (5) muhimu. 1. RAM Boom J8 ina RAM GB 2 hivyo huipa simu uwezo wa kuendesha mifumo yake yote kwa kasi sana, hii ni nzuri tena inavutia kwasababu hakuna kitu kinachoudhi kama simu kwenda taratibu kila ukitaka kufungua faili lazima upoteze muda. BoomJ8 ni suluhisho la kuokoa muda wako. 2. CAMERA Kamera ya nyuma ina MP13 (na flashi) na camera ya mbele ina MP5 (Pia pamoja na flashi hapa ni full selfie), Picha zake ni angavu sana. 3. Intafesi yake Boom J8 ina intafesi mpya ambayo pia husaidia kuboreshwa kwa uwezo wa simu yako. 4.Hedifoni zake Ukiziona hedifoni za Boom J8 utashangaa, zimetengenezwa kwa malighafi ya ngozi laini sana ambayo ina mwonekano wa kifasheni, hizi ziko pamoja na mashine yenyewe Boom J8. Sauti inayotokana na Headifoni za Boom J8 haichoshi masikio kusikiliza midundo kwasababu imetengenezwa kitaalam kiasi cha kuchuja mikwaruzo yote na kufanya midundo nyororo. 5. Wembamba Boom J8 ina mvuto wa wembamba ambapo upana wa wembamba wake mm7.35 na fremu yake ni mm3.5. Kwa ufupi wembamba wa Boom J8 ni sawa na vipande 20 vya karatasi za rimu au gazeti. Inaleta wepesi wa kuishika vizuri kwa mkono mmoja, inabebeka yaani ni 'Portable' Ni midundo kwa kwenda mbele ukiwa na Boom J8. Boom J8 inanunulika, Uzuri wa Boom J8 inaweza kumilikiwa na mtu yeyote, unanunua, unaimiliki kiganjani, unahisi ufahari na unakuwa wa kisasa zaidi na uhuru wa kuishika mbele ya mtu yeyote!