Malecela atoa somo kuepuka njaa Dodoma


Dodoma. Makamu Mkuu wa Rais mstaafu, John Malecela
ameishauri Serikali kutilia mkazo kilimo cha umwagiliaji katika Mkoa wa Dodoma. Malecela aliyasema hayo wakati Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alipofanya ziara ya kukagua skimu ya umwagiliaji ya zabibu ya Chinangali II, Chamwino, yenye jumla ya ekari 1,250. Amesema iwapo Serikali itafanya hivyo itausaidia mkoa huo kuondokana na njaa ambayo huwa inaukabili mara kwa mara. “Serikali inaingia gharama kubwa sana kuanzisha skimu za umwagiliaji, lakini nyingi zinakosa ufuatiliaji na uongozi imara matokeo yake zinakufa,”amesema. Ametoa mfano skimu ya Mgangalenga iliyopo Mpwayungu Wilaya ya Chamwino yenye zaidi ya ekari 20,000.