Manji afika polisi


Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha
Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada yaa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi. Picha na Muyonga Jumanne Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi. Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo. Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya Ijumaa. Manji amewasili na gari aina ya Range Rover rangi nyeusi.