Yanga yapewa vibonde Kombe la FA


Dar es Salaam. Ratiba ya raundi ya sita ya Kombe la Shirikisho (ASFC) imewekwa hadharani huku mabingwa watetezi wa michuano hiyo,
Yanga wakipangwa kukutana na Kiluvya United ya Pwani. Kiluvya ilitinga hatua ya sita bora kwa kuichapa Ruvu Shooting kwa mabao 2-1 huku Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo wikitinga hatua hiyo baada ya kupata kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ashanti. Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema Yanga iko tayari kucheza na timu yoyote bila kujali udogo au ukubwa wa timu husika. “Nimeiona lakini ushindani ni ushindani, sisi tunaweza kucheza na timu yoyote iwe Simba, Kagera au Kiluvya tuliyopangwa nayo, hatuna hofu,” alisema Hafidh. Ratiba hiyo pia inaonyesha Simba itacheza na African Lyon, Kagera itaikaribisha Stand United, Mighty Elephant itacheza na Ndand wakati Azam FC itakuwa kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi kucheza na Mtibwa Sugar. Michezo mingine ni Madini FC itakayovaana na JKT Ruvu, Mbao FCc itapambana na Toto Africans, Tanzania Prsions itacheza na Mbeya City jijini Mbeya. Hata hivyo, klabu za Ligi Kuu zimeonekana kutawala kwenye michuano hiyom ambaypo kati ya timu 16 zilizofuzu hatua hiyo, timun 13 zinashiriki Ligi Kuu. Michezo ya hatua ya 16 itachezwa kati ya Februari 24 na Machi 7. Bingwa wa michuano ya FA ataiwakilisha nchi katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

By Fredrick Nwaka