Harmonize -amkacha harmorapa-Adaiwa Kumtukana Live Meneja wa Harmorapa

Harmonize Adaiwa Kumtukana Live Meneja wa Harmorapa Wakiwa
Studio ni madai mazito!
Taarifa iliyotolewa na Kituo cha East Africa Television kupitia ukurasa wao wa Twitter imeeleza kuwa, Msanii kutoka WCB, Harmonize ilikuwa awepo kwenye kipindi cha FNL cha televisheni hiyo usiku huu (Ijumaa Machi 24, 2017), lakini ameingia mitini baada ya kumuona meneja wa msanii Harmorapa maeneo ya studio hizo.
Inadaiwa kuwa baada ya kumuona meneja wa Harmorapa, msanii Harmonize amemuoneshea kidole cha kati ambacho hudaiwa kuwa ni ishara ya tusi kisha akaondoka maeneo ya studio hizo.
 Aidha Harmorapa amelaani kitendo hicho cha udhalilishaji na kudai kuwa Harmonize amemtukana bosi wake kwa kumuonyesha ishara ya kidole cha kati baada ya kukutana.
Kwa upande wao, kituo cha EATV, kupitia akaunti yao nya Twitter kimeomba radhi kwa watazamaji wake wote kutokana na kitendo hicho cha aibu kilichofanywa na msanii huyo akijaribu kuelezea kilichotokea