MAGUFULI AZINDUA MAGARI 580 YA DANGOTEUzinduzi wa magari ya kiwanda cha saruji cha dangote mtwara umefanyika leo mjini mtwara ukiwa umehudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo waziri wa nishati na madini profesa muhongo.
Raisi magufuli ameziainisha changamoto kadhaa na ukiritimba uliopo baina ya watendaji na kampuni zilizo aminiwa ambazo zimeonekana kukwamisha juhudi mbalimbali za maendeleo ya kiwanda hicho
Raisi magufuli amemshukuru alhaji dangote kwa uwekezaji wake katika nchi ya Tanzania kwani kiwanda hicho kimetoa nafasi za ajira za moja kwa moja takribani 800 na jumla ya ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja ni elfu ishirini
Pia amemshukuru Raisi kikwete na uongozi wa awamu ya nne kwa juhudi kubwa za ufanilishaji wa uwekezaji wa kiwanda hicho ambao umewezasha serikali kukusanya jumla ya mapato ya shilingi bilioni 46 za kitanzania tangu kilipoanza uzalishaji tarehe 16/2/2016 baada ya kuzinduliwa tarehe 10/10/2015
kiwanda cha saruji cha dangote kinatarjiwa kudhalisha tani milioni tatu za saruji kwa mwaka hali itayopelekea ukusanyaji wa mapato wa bilioni 136 kwa mwaka serikalini
aidha raisi magufuli amezitaja changamoto zilizopo na zilizokuwepo katika kiwanda hicho kuwa ni
     Magari yalikaa miezi miwili bandarini baada ya kufika na yalitoka siku moja baada ya mimi kupiga simu “hivyo nikabaini kuna  tatizo hapa” alisema
     upatikanaji wa mali ghafi kwa maana ya makaa ya mawe na gesi kwani shirika la NDC lililopewa dhamana ya uzalishaji wa makaa ya mawe halikufanya kazi yake badala yake kuingia mkataba na shirika lingine la TAN COAL ili kuchimba makaa ya mawe ambalo shirika hilo pia limekuwa kikwazo kwa upatikanaji wa mali ghafi za kutosha kutumika katika kiwanda cha saruji hivyo Raisi magufuli ameamrisha serikali kutoa kibali kupewa eneo la kuchimba makaa ya Mawe kwa alhaji dangote ili ili kuondoa hali hii kwa makampuni hayo ambayo ameyaita ni ya kitapeli aidha profesa muhongo amemuahidi Raisi wa jamuhuri ya muungano  masuala hayo kufanyiwa kazi hadi kufikia jumatano ya wiki ijayo
    changamoto ya gesi kudhalishwa mtwara kisha kusafirishwa kilomita miatano mpaka jijini Dar-Es-Salaam na kasha kurudishwa tena mtwara kuuzwa jambo ambalo linaongeza gharama ya malighafi hiyo badala kupatikana palepale mkoani mtwara kiasi cha kilomita 5 hadi 6
     Raisi ameitaja changamoto ya nafasi za ajira kwa wazawa hasa za udereva kwani kumekuwa na kampuni nyingine katikati ya upatikanaji wa ajira kiwandani hapo inayofikia kupokea hata rushwa ili kupata ajira kwa watumishi hali iliyo wasilishwa na mwakilishi wa madereva aliyepewa nafasi ya kueleza hali ya ajira kiwandani hapo “kwani ajira za madereva zilitangazwa zaidi ya miatanao tuliitikia wito usaili na mafunzo ya awali yalitolewa tukisubiri kuitwa hadi sasa hakuna dereva aliyeitwa kiwanda kinatumia magari ya kukodi baadhi ya watu wameazisha kampuni ili kufanya kazi”  amesisiitiza muhindi ambaye ana magari zaidi ya miambili ni kama ameanzisha kampuni ya dangote B ndani ya kampuni inayomilikiwa na hao wanaofanya udalali je wahindi wanafanya nini Akisitiza wachunguze hata uhalali wa uraia wao Raisi ameahidi suala hilo kufanyiwa kazi na akielekeza watendaji wake kufanyia kazi maamuzi ya mambo kama hayo mapema na sio kumsubiri yeye
Raisi amezindua magari hayo yatakayotumika kiwandani hapo yakitarajiwa kutoa ajira zaidi ya miatano kwa kukata utepe pamoja na alhaji dangote