AFC Arusha haiuzwiArusha. Katibu Mkuu waAFC Arusha, Charles Mwaimu amesema timu hiyo haiuzwi na hawana mpango wa kumuuzia mtu kwa
sasa, zaidi ya kujiandaa mapema na ligi daraja la pili (SDL) msimu ujao.
Kauli hiyo ya Katibu Mwaimu inatokana kuwepo kwa taarifa kuwa viongozi wa AFC wanataka kuuza timu bila kushirikisha wananchi wenye timu yao.
“Sisi ni viongozi tu tumepewa dhamana ya kusimamia kama watoto wa nyumbani na hatuma mamlaka yoyote ya kuiuza hivyo wenye sauti kubwa ya kuuza au kutoiuza timu ni wananchi wenye timu yao na siyo viongozi.”
“Wiki mbili sasa taarifa zinazidi kuenea kila kona ya jiji la Arusha kuwa AFC inauzwa, lakini hupati taarifa sahihi nani anauza na kwanini tuuze hii timu,” alisema Mwaimu.
Mwaimu alisema lengo la kuingia kambini mapema ni kuepuka kutoa lawama za kila siku, kuwa wameshindwa kufanya vizuri kwa kisingizio cha kuchelewa kufanya maandalizi mapema.


By Yohana Challe