Dodoma.
Wabunge wa CCM wameitaka Serikali kutoa majibu sahihi bungeni kuhusu
utambulisho wa mtu aitwaye Daudi Bashite.
Sakata
hilo liliibuka
juzi katika kikao cha wabunge wa CCM kilichoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa mjini hapa.
Wabunge
tofauti waliozungumza na Mwananchi walisema kuwa, suala hilo lilihojiwa kwenye kikao hicho cha ndani
ambacho hufanyika kabla ya mkutano wa Bunge kwa ajili ya kuwekana sawa.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, wabunge hao walidai kuwa Serikali imeendesha na
inaendelea kuhakiki vyeti vya elimu na baadhi ya watumishi wameshakumbwa na
adhabu au kufukuzwa kazi kwa tatizo la vyeti feki.
Mpashaji
mwingine aliiambia Mwananchi kuwa, Waziri Mkuu alijibu kuwa Serikali imepokea
hoja hiyo bila kutoa ufafanuzi zaidi.
Pamoja na kelele za
watu tofauti kueleza uwezekano wa kughushi vyetu, si Baraza la Mitihani
(Necta), Polisi wala Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
iliyojitokeza kuzungumzia suala hilo
au kuchukua hatua.
Comments
Post a Comment