NMB HASARA TUPU KWA BUNGE


BAADA YA MAJIGAMBO YA HAPA NA PALE KATIKA MAKABIDHIANO YA VIFAA VYA MICHEZO VYENYE THAMANI YA
SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI SABA KUTOKA NMB VIKIKABIDHIWA NA MKURUGENZI WA WATEJA WADOGO NA WA KATI BENKI YA NMB BW.ABDUL MAJID NSEKELA KWENDA KWA TIMU YA BUNGE HAPO JANA KUELEKEA MPAMBANO WENYE NIA YA KUDUMISHA MAHUSIANO BAINA YA BENKI YA NMB NA WABUNGE WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. JEZI HIZO ZILITOLEWA KWA TIMU TATU ZA SOKA, MPIRA WA PETE NA MPIRA WA KIKAPU MH. WILLIAM NGELEJEJA ALIJITAPA KUWA KWA MARA TISA WALIZOWAHI KUKUTANA NA NMB, NMB HAIJAWAHI KUSHINDA HUKU KOCHA WA BUNGE SPORTS CLUB VENANCE MWAMOTO AKIJINASIBU ILIKUWA LAZIMA KUSHINDA KWA KUWA VIFAA WALIVYOKABIDHIWA VITALALA KWA MAJI MAREFU KABLA YA MPAMBANO WAKATI HUO HUO NAHODHA WA NMB RICHARD MWALIBA AKIJITAPA HATA VIFAA VILALE KWA NANI NI LAZIMA WASHINDE. LEO HII KIPUTE KIMEPIGWA NA HATIMAYE BUNGE KUIBUKA KIDEDEA KWA KUICHABANGA NMB MABAO MAWILI KATIKA UWANJA WA JAMHURI. MABAO YA BUNGE YALIWEKWA KIMIANI NA MOHAMED MCHENGERWA NA GOLI LA PILI LILIWEKWA KIMIANI NA COSATO CHUMI (GAZZA)