Mh. Ridhiwan Kikwete akabidhi Msaada


Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwan Kikwete akabidhi Msaada wa vitanda vya kujifungulia (5), vitanda vya wodini (20), Magodoro 20 na mashuka 50 kwa Halmashauri ya Chalinze ambavyo vitagawiwa katika vituo vya Afya 5 vilivyo katika Tarafa 5 za Halmashauri ya Chalinze . Vifaa hivi ni sehemu ya Utekelezaji wa Ahadi za Mheshimiwa Raisi wetu na Ilani ya CCM -2015 kwa Wananchi wa Halmashauri ya Chalinze.