Anayesema Ninatumia Unga Anipeleke Soba-amber

Msanii na muuza nyago kwenye video za Bongo Fleva, Lulu Augen ‘Amber Lulu’.
MSANII na muuza nyago kwenye video za Bongo Fleva, Lulu Augen ‘Amber Lulu’, amefunguka kuwa
wanaomsema anatumia madawa ya kulevya ‘unga’, basi wampe­leke sober house (nyumba ya kusaidia waathirika wa unga) ili akapatiwe tiba.
Akizungumza na 3-Tamu, Amber Lulu alisema kuwa anavyojua teja wa unga huwa hajifichi hivyo kama kweli anatumia, ipo siku itadhihirika kuliko kila siku kuse­mwasemwa juu ya jambo ambalo hausiki nalo.
“Nimekuwa nikisemwa kila siku kuwa ninatumia unga, sasa nasema kama kuna mtu ana uhakika na hilo, basi anipeleke sober house nikatibiwe. Ni vyema watu wakajua kuwa hata mimi ni binadamu, ninaumizwa na kuse­mwasemwa,” alisema Amber Lulu.