Magufuli amsubiria Nkurunziza

Kagera .Rais John Magufuli amewasili katika uwanja wa  mpira wa Lemela Kata ya 
Kanazi  Wilaya Ngara  Mkoani Kagera ambapo atampokea Rais wa Burundi  Pierre Nkurunziza na baada ya hapo watakagua gwaride.
Mara baada ya kumaliza ukaguzi wa gwaride hilo viongozi hao watakuwa na maongezi maalum.
Rais Magufuli yuko ziarani Kanda ya ziwa na jana alizindua barabara ya kiwango cha lami ya Kagoma- Biharamulo-Lusahunga.
Pamoja na uzinduzi Rais Magufuli pia alihutubia wananchi ambako umati mkubwa umehudhuria uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 154.