Mke wa Mugabe ataka mumewe ateue mrithi


Grace  Mugabe  amevunja  des
turi  mojawapo kubwa  ya  Chama  cha  Zanu  PF,  kwa  mshangao kwa  kumtaka  mumewe huyo  mwenye  umri wa miaka  93  amteua  mrithi  wake. Mwanamama huyo ambaye ni mwenyekiti  wa tawi  la  wanawake  la  Zanu  PF  alisema  hayo  jana alipokuwa  akihutubia  kikao  cha  Umoja  wa Wanawake  kwenye  makao  makuu  ya  chama hicho  mjini  Harare. Grace  alijaribu  kutumia  Biblia  katika  rai  yake alipozungumzia  fumbo  la  Adonija  aliyeandaa hafla  ya  kujitawaza  yeye  mwenyewe  kwa  kuwa mfalme  baba  yake  alikuwa  mgonjwa.  Kichekesho ni  kwamba  hata  Mugabe  ni  mgonjwa,  amekuwa akifanya  safari  za  Asia  kupata  matibabu. Kadhalika  Grace  alinukuu  kitabu  cha  2Samuel: 9-1  kwamba  “Kisha  Daudi  akasema,  Je,  amesalia mtu  mmoja  katika  nyumba  ya  Sauli,  nipate kumtendea  mema  kwa  ajili  ya  nyumba  ya Jonathan.” Grace  ametoa  kauli  hiyo  wakati  makundi  ya wanasiasa  mashuhuri  yakipigana  vikumbo  kutaka kumrithi  Mugabe  ambaye  ameongoza  nchi  tangu uhuru.