Ajali ya basi yaua wawili

Basi la kampuni ya Sharon lililokuwa likitoka
Dodoma kwenda Arusha, limepinduka eneo la mabanzini mjini Babati na kusababisha vifo vya watu wawili huku wengine wakijeruhiwa.
Majeruhi wa ajarili hiyo wamepelekwa hospitali ya Mrara mjini Babati.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara akizungumza na gazeti hili, Francis Massawe akizungumza juu ya ajali hiyo alisema kondakta na mtoto mdogo ndiyo walifariki.