MBUNGE WA CHALINZE MH:RIDHIWANI KIKWETE AGAWA VIFAA VYA MICHEZO


Mbunge wa Chalinze ijumaa hii
 amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo la chalinze zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya bagamoyo. Sherehe hizo zilizofanyika kimange zilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Madiwani wote wa Jimbo la Chalinze na watendaji wao wa kata ambao walipokea jezi kwa niaba ya timu zao.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye muandaaji mkuu wa mashindano hayo akishirikiana na wabunge wa majimbo yote Pamoja na kugawa jezi , mbunge wa chalinze aliwaahidi kuwapatia mshindi wa pili wa mashindano Pilkipiki ya Miguu miwili, na jezi kwa timu zote Tatu za juu kufuatia mkuu wa wilaya kuwachangia mshindi wa kwanza pikipiki ya Toyo ya miguu mitatu ili itumike kwa shughuli za kipato kwa vijana.