Dereva wa Mbunge John Heche Avamiwa, Akatwa Mapanga

DEREVA wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, John Heche (Chadema) amevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumkata kwa mapanga usiku wa
kuamkia leo majira ya saa 2 usiku huku ikielezwa kuwa hali yake siyo nzuri.
 Taarifa hizo za kusikitisha zimethibitioshwa na Bosi wa Dereva huyo ambaye ni Mbunge John Heche kupitia Katibu wake, Mrimi Zablon ambaye amekiri kuwa dereva huyo anayefahamika kwa jina la Suez Daniel Maradufu ni kweli amepata shambulio hilo na sasa yupo hospitali akipatiwa matibabu.

Jana majira ya saa mbili usiku dereva wa mbunge Mh. John Heche anayejulikana kwa jina la SUEZ DANIEL MARADUFU alivamiwa na watu wasiojulikana na kushambuliwa kwa kukatwa katwa na mapanga kichwani na hali yake si nzuri, anaendelea na matibabu kwenye Hospitali ya Bomani Tarime.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Tarime Vijijini
15/9/2019.