SANCHI ADAI KUKAA NUSU UTUPU KUMEMPA MCHUMBA

MWANAMITINDO Jane Rimoy ‘Sanchi’ ambaye
amejizolea umaarufu kutokana na uvaaji wake wa nguo zinazomuonesha akiwa nusu utupu, amefunguka kuwa, pamoja na kwamba watu wanampiga vijembe na kumuona mwanamke asiyefaa kutokana na uvaaji wake huo, lakini ukweli ni kwamba ndiyo umempa mchumba.

Sanchi aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, anashangaa watu wanavyombeza wakati yeye ni mwanamitindo hivyo hakuna cha ajabu katika vazi lake lolote na ndiyo maana mwanaume ambaye anataka kumchumbia, amemchagua na kujua wazi anafaa kuwa mke. “Watu hawaelewi maana ya uanamitindo.

Ndiyo maana wanaweza kukusema bila kujua. Kama ingekuwa ni kinyume cha maadili, basi hata mchumba asingejitokeza,” alisema Sanchi.