INASIKITISHA! BINTI ALIYEKATWA MIGUU, AMLILIA MAGUFULI – VIDEO

Binti Gladness Fidilish mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Mtaa wa Mji Mwema wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, amemuomba Rais John Magufuli na Watanzania kumsaidia kupata miguu bandia baada ya kupata ajali iliyopelekea miguu yake kukatwa.

Ajali hiyo ilitokea Julai 19.2017 baada ya pikipiki aliyokuwa amepanda kugongwa na Basi katika eneo la Round-About ya CCM jijini Mwanza ambapo ilipelekea kukatwa miguu hiyo. Amesema licha ya dereva aliyemgonga kukamatwa lakini baadaye aliachiliwa kwa madai kuwa dereva wa pikipiki ndio alikuwa mwenye makosa. Hivyo binti huyo ameachwa bila msaada.

Gladness amesema kuwa baada ya kukatwa miguu hiyo familia yake ilifanya jitihada za kumtaftia miguu bandi lakini wameshindwa kununua miguu hiyo kutokana na gharama kuwa kubwa. Irene Fedha dada yake Gladness amesema kuwa tangu mdogo wake akatwe miguu amekuwa akiteseka kutokana na kushindwa hata kwenda haja.

Kwa upande wake jirani wa familia hiyo Bi. Magret Christopher amesema kuwa msichana huyo anahitaji msaada wa hali na mali ili kupata miguu bandia.