UKATILI WALIOFANYIWA WATUMWA KUTOKA AFRIKA HUKO AMERIKA

Mgongo wa mtumwa kutoka Afrika uliojaa makovu ya kuchanwa kutokana na kuchapwa mijeledi wakati wa kufanyishwa kazi za kitumwa.
Watumwa na watoto wao wakifanyishwa kati katika shamba la pamba.
…Wakivuna pamba.
…Wakiwa wamepangwa kwa ajili ya kununuliwa mnadani.
Kazi ya kuvuna pamba ikiendelea katika mojawapo ya mashamba.
Hapa ni kwenye mnada wa watumwa.
Mzungu Joseph Carpenter aliyepiga vita utumwa, akiwa na mtoto wa familia ya watumwa.
Mtumwa Samuel Harper na mkewe wakiwa Ontario, Canada, baada ya kutoroka kutoka Marekani.
Moja ya wakazi waliyokuwa wanalundikwa watumwa.
PICHA za kusikitisha zilizopigwa miaka zaidi ya 150 iliyopita zinaonyesha ukatili wa kutisha waliokuwa wanafanyiwa watumwa kutoka Afrika waliosombwa kupelekwa barani Amerika kwenda kufanyishwa kazi ngumu.

Huko walichapwa mijeledi, wakafanyishwa kazi nzito kama wanyama kwenye mashamba ya pamba na miradi ingine migumu wakitishwa kwamba polisi wangewasaka popote na kuwakamata iwapo wangethubutu kutoroka.

Picha hizo zimeibuliwa katika kumbukumbu ya kutimia mwaka wa 153 tangu kupigwa marufuku kwa utumwa nchini Marekani, Januari 1, 1865 kufuatia Badiliko la 13 la Katiba ya nchi hiyo ambalo lilisainiwa na Rais Abraham Lincoln, Februari 1, 1865.

Miongoni mwa picha hizo ni pamoja  na zilizopigwa mnamo miaka ya 1700 zikionyesha maisha ya watumwa nchini Marekani ambapo kuna moja inayoonyesha mgongo wa mtumwa ulivyochanwa kwa mijeledi na picha nyingine nyingi zikionyesha wakifanya kazi za kitumwa kwenye mashamba ya pamba.

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI