SERENGETI BOYS MABINGWA AFRIKA MASHARIKI


Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys imeibuka Bingwa wa Mashindano ya CECAFA U-17 baada ya kuichapa Somalia kwa mabao 2-0 katika fainali iliyopigwa jana nchini Burundi. Serengeti Boys ilionyesha kiwango cha juu cha soka katika mchezo huo wa fainali ambapo hadi mapumziko ilikuwa ikiongoza kwa bao moja. Bao la pili la Serengeti boys lilifungwa katika kipindi cha pili. Mabingwa hao wapya wa Afrika Mashariki na Kati, wamekabidhiwa kombe hilo na mgeni rasmi wa fainali hiyo ambaye ni Rais wa shirikisho la soka barani Africa Ahmed Ahmed. erengeti Boys walitinga fainali hiyo kwa kuwafunga Kenya U17 kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa Alhamisi huku Somalia wakiingia kwa kuifunga Uganda 1-0. Katika hatua ya makundi, Serengeti Boys ilifanikiwa kuzichapa Sudan na Uganda huku timu ya taifa ya vijana ya Zanzibar, Karume Boys ikiondolewa kutoka na kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa.